Wananchi wengi wa Marekani wamekumbwa na mshangao na hawaamini kilichotokea kwenye uchaguzi uliomalizika na kumpa ushindi Donald Trump ambaye atakua Rais wa 45 wa taifa hilo, pamoja na ushindi huo Trump anakutana na changamoto za kupingwa na maelfu ya Wamarekani.
Wamarekani
wengi wameingia barabarani na kupiga kelele za kupinga ushindi wa Trump
kwa kudai kuwa huyo sio Rais waliyemchagua, ikumbukwe kuwa mpaka sasa
kwa mujibu wa kura zilizopigwa na raia wa Marekani zinaonesha Hillary
Clinton anaongoza kwa kupata kura nyingi.
Sasa
sheria za uchaguzi nchini humo zinasema ili mgombea aweze kutangazwa
mshindi wa kiti cha Urais inatakiwa pamoja na kura za wananchi ni lazima
apate kura za wajumbe 270 au zaidi kati ya wale 538 Wajumbe kutoka
Majimbo mbalimbali na ni kitu ambacho Donald Trump amefanikiwa kukipata
pamoja na kuwa kura za wananchi zilikua pungufu kwake.
Baada ya
kuwepo maandamo ya siku ya pili mfululizo kumtaka Trump aachie nafasi
hiyo, Rais huyo mteule ameandika kwenye Twitter account yake kuwa watu
wanaofanya hivyo wanashinikizwa na vyombo vya habari wakati wakijua kuwa
yeye ni mshindi halali na hawamtendei haki.
‘Nimekua
na uchaguzi wenye mafanikio na uwazi, sasa Waandamanaji wanaoshinikizwa
na vyombo vya habari wanaandamana, hii sio haki…’ – Trump
Kwenye Tweet nyingine Trump aliandika jinsi alivyokua na siku nzuri
Washington DC walipokutana na Rais Obama kwa mara ya kwanza, kilikua ni
kikao kizuri… Melanie (Mke wake) amevutiwa sana na mke wa Rais Obama.
No comments:
Post a Comment