Huwa anazunguka mitaa ya mji wa Abuja akiwatafuta wateja ambao wangependa viatu vyao kushonwa au kupakwa rangi.
Idris hana kisomo lakini hajutii hilo. Anasema kuwa hupata karibu dola 5
kwa siku na kuongeza kuwa kipato chake cha mwezi mzima ni cha juu
kuliko cha wafanyakazi wengine wa umma, ambao mishahara yao ni kati ya
dola 125 na 190.
Ndoto ya Idris ni kumiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza rangi ya
viatu, lakini kwa sasa ameamua kuwa mpaka viatu rangi kwenye mitaa ya
mji wa Abuja.
Toa maoni yako.
No comments:
Post a Comment