Thursday, November 17, 2016

uandikishwaji vitambulisho vya Taifa kuanza upya desemba 2016




h3h9417
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba



Serikali imesema utambuzi na uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa utaanza upya Desemba mwaka huu ili kusaidia kupunguza utitili wa vitambuliso . 


Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba , zoezi hilo litasaidia kutoa suluhisho la kudumu la mishahara hewa kwa watumishi wa umma.

“Kuna watu wanatumia majina tofauti lakini kwa kutumia njia ya kielekrotoniki, alama za vidole zinatofautisha tunaamini kutumia alama za vidole ataendelea kutumbulika,”alisema Waziri Nchemba.

Amesema lengo la kufanya hivyo kwenye vitambulisho hivyo vitasaidia maeneo mengi kama bodi ya mkopo, mifuko ya jamii pia anaamini kutakuwa na uhusiano mzuri.

Ameongeza kuwa baada ya zoezi la watumishi wa umma wanakwenda kuendelea kutoa namba za utambuzi kwa wananchi na ‘data base’ tayari ipo waliyopewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Taasisi zitatumia utambuzi huu na zaidi ya taasisi 35 zimeanza kutumia taarifa zake kutoka NIDA na zingine zaidi ya 70 zimeonyesha nia ya kutumia taarifa hizo,”alisema.

Kwa upande wa NIDA, usahili wa awali walihakiki watumishi wa umma nchi mzima wapatao laki 565,000 na wengine bado kutokana na sababu mbalimbali.

Hadi sasa wamesajili wananchi milioni 3,900,000 na vitambulisho vya taifa milioni 2,700,000 ambavyo tayari vimezalishwa.
 
Toa comment zako.
 
 

No comments:

Post a Comment