Tuesday, November 15, 2016

Rick Ross kuuza nyumba yake kwa bei ya hasara baada ya kukosa mteja



rick-ross-birthday 

Hali ya kiuchumi ya rapper Rick Ross inazidi kuwa mbaya – baada ya kukosa mteja wa kununua nyumba yake ya mjini Florida sasa ametangaza kuiuza kwa bei ya hasara.

 Mtandao wa TMZ, umeripoti kuwa rapper huyo ametangaza kuuza nyumba hiyo kwa kiasi cha dola milioni 1.3 wakati hapo mwanzo alitangaza kuiuza kwa kiasi cha dola milioni 1.5.

Nyumba hiyo yenye vyumba 6 vya kulala, mabafu 5, jiko kubwa, studio mbili za kurekodi aliinunua mwaka 2008 kwa kiasi cha dola milioni 1.25 na itakuwa ni nyumba yake ya pili kuiuza kwa mwaka huu baada ya ile ya kwanza aliyoiuza kwa kiasi cha dola milioni 6.

Siku chache zilizopita tovuti ya TMZ imeripoti kuwa IRS inamdai bosi huyo wa MMG karibu dola milioni 5.7 za kuanzia mwaka 2012 hadi 2014.


No comments:

Post a Comment