Jarida la ‘People’ limemtaja mwanaume mwenye mvuto zaidi Duniani mwaka 2016.
November 15 2016 Jarida maarufu la nchini Marekani People limemtangaza mwanaume anayeaminika kuwa na mvuto zaidi duniani kwa mwaka 2016 ambapo limemtaja staa mwigizaji Dwayne ‘The Rock’ Johnson kuwa ‘The Sexiest man alive’ ama mwanamume mwenye mvuto zaidi kwa mwaka 2016. Jarida hilo liliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema…..
‘Ni mpole, mtanashati na aliyejengeka kimwili’
Baadae kupitia ukurasa wake wa Twitter, The Rock alitoa shukrani zake kwa jarida hilo pamoja na Mashabiki juu ya ushindi huo.
Mwaka 2015 nafasi hiyo ilikuwa imeshikwa na David Beckham
Ni dhahiri kwamba 2016 umekua mzuri sana kwa The Rock, kwani licha ya kutajwa kuwa Mwanamume mwenye mvuto zaidi duniani, jarida la FORBES lilimuandika kuwa muigizaji aliyeingiza pesa ndefu zaidi kuanzia June 2015- 2016 huku akiwa ametengeneza dolla za kimarekani milioni 64.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 14 za kibongo.
No comments:
Post a Comment