President and CEO of WORLD FOOD CHAMPIONSHIP Mr Mike Mc Cloud akimkabidhi tuzo Uisso
Mtanzania Fredy Uisso aliyekwenda Alabama, Marekani,kushiriki
mashindano ya upishi ameibuka mshindi wa nne katika mashindano hayo ya
kidunia.
Chef Uisso ambaye ni mpishi mwandamizi katika mgahawa wa Afrikand uliopo Kinondoni, anaandika historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kushiriki fainali za mashindano hayo na kuibuka kuwa mshindi wa nafasi hiyo huku akiwabwaga wapishi 21 kutoka hoteli kubwa na maarufu duniani walioshiriki fainali hizo zilizoanza Novemba 8 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment