Kesi ya kutuma ujumbe wa uchochezi dhidi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema na mke wake Neema Lema imeshindwa kusikilizwa leo baada ya mbunge Lema kushindwa kuletwa mahakamani kutoka Rumande.
Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo Augustino Rwezire ametaka upande wa waendesha mashtaka kuhakikisha kesho mshtakiwa analetwa mahakamani ili kesi yake iweze kusikilizwa.
Wakili wa CHADEMA John Malya amesema mahakama iliamuru ndani ya saa moja aweze kuletwa lakini ikashindikana………
>>>’Ilipaswa Lema aletwe mahakamani lakini Jamhuri inayomshtaki haikufanya jitihada kupeleka nyaraka za kimahakama gerezani ili atoke, kwa hiyo mimi nikaenda mahakamani nikaomba hizo nyaraka mheshimiwa akawapa jamhuri saa moja wamfuate Lema wamlete, magereza wakasema wao hawana gari’
No comments:
Post a Comment