Monday, November 21, 2016

Mwanamke anayejiita 'mungu' aliyewapiga watu risasi India

Sadhvi Deva Thakur mara nyingi huonekana ameshika bunduki 


Polisi nchini India wanamtafuta Sadhvi Deva Thakur, mwanamke aliye mafichoni baabda ya kufyatua risasi za kusherehekea kwenye harusi

Shaghaziye bwana harusi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.

Kwenye video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katika jimbo la Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur anaonekana akifyatua risasi akitumia bunduki aina ya revolver.

Hakuna mengi kumhusu Sadhvi

Baadhi ya walinzi wake nao wanaonekana wakifyatua risasi.

Vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa Sadhvi, ambalo ni jina la kiindi linalomaanisha mwanamke aliye mtakatifu au anajiita kuwa mungu alingia sakafuni, ambapo alimuomba DJ kucheza wimbo aliotaka na akaanza kucheza densi.

Wakati huo ufyatuaji risasi ulikuwa ukiendelea.

Ripoti zinasema kuwa familia za bibi na bwana harusi zilimuomba awache maombi yao yaliambulia patupu.

Ni wakati shangaziye bwana Harusi mwenye umri wa miaka 50 alianguka baada ya kupigwa risasi na wengine watatu kujeruhiwa vibaya, ndipo ufyatuaji huo ukasitishwa.

Wakati huo Sadhvi na walinz wake sita walitoweka. Polisi wamewafungulia kesi ya mauaji na wanajaribu kuwatafuta watu hao saba.

Toa maoni yako.

No comments:

Post a Comment