Tuesday, November 15, 2016

Anajua kuchana, kutengeneza hits, lakini hiki ni kitu rahisi ambacho Joh Makini hawezi kufanya

14677234_1778515885735369_4096863772012969984_n 
Joh Makini kwa sasa ni jina ambalo huja haraka akilini kwa Watanzania wengi wanapoombwa wamtaje msanii wa hip hop mwenye mafanikio.

Yeye mwenyewe anajiita ‘Rap King.’ Lakini licha ya uwezo mkubwa wa kuandika mashairi, kuchana kwa style nyingi na kutengeneza hits kibao, kuna kitu rahisi kabisa ambacho amekiri kuwa hawezi kufanya.

Joh Makini hajui kupika!

 Ametoa siri hiyo alipotakiwa kwenye kipindi cha Coke Studio kutaja kitu kimoja ambacho watu hawajui kuhusu yeye. Rapper huyo ameungana na mwenzake wa Nigeria, Falz kutengeneza pair kwenye show hiyo.
 

No comments:

Post a Comment