Wasiyemtaka ameingia ikulu ya Marekani na kama walikuwa wakidhani
vitisho alivyokuwa akivitoa wakati wa kampeni vilikuwa ni mkwara tu,
wanapaswa kujipanga upya!
Ni kwasababu Rais Mteule wa nchi hiyo, Donald Trump ameusisitizia
msimamo wake dhidi ya wahamiaji haramu nchini humo. Amedai kuwa ana
mpango wa kuwafungashia virago wahamiaji haramu takriban milioni
tatu,hasa wale wenye rekodi ya uhalifu.
Amesisitiza pia kuwa mpango wa kujenga ukuta upo pale pale.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ashinde uchaguzi na kuja
kuchukua kijiti cha Urais toka kwa Barack Obama, Trump amewahakikishia
wafuasi wake kuwa atawatimua wahuni na wauzaji wa madawa ya kulevya wote
toka Marekani.
Katika mahojiano kwenye kipindi cha CBS, 60 Minutes, Jumapili jioni,
Trump amesema atajenga ukuta kutenganisha Mexico na Marekani kama
alivyoahidi kwenye kampeni yake.
Kuna wahamiaji haramu takriban milioni 10 nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment