Tuesday, November 15, 2016

Nchi 10 hatari kuzitembelea duniani, Bara la Afrika ni zaidi

 


November 15, 2016 nimeipata list ya nchi zilizotajwa kuwa hatari zaidi kuzitembelea duniani na taasisi ya utafiti ya International SOS and Control Risks. Nchi zilizotajwa kuwa hatari zaidi ni Syria, Afghanistan na Yemen huku Norway, Sweden na Iceland zikiwa ni nchi salama zaidi duniani.
Syria
Afghanistan
Yemen
Libya
Sudan
Somalia
Mexico
Colombia
Pakistan
Egypt

Imeelezwa kuwa asilimia 72% ya watu duniani wanaamini kuwa hatari katika nchi nyingi imeongezeka zaidi kuanzia mwaka 2016 na sababu ikiwa ni matukio ya ugaidi na magonjwa huku Bara la Afrika likitajwa kua na maeneo mengi zaidi hatari, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ipsos Mori.

Ndani ya mwaka mmoja wananchi wamesema kuwa matukio ya ugaidi na kusambaa kwa virusi vya Zika kumefanya kupungua kwa safari za watalii katika maeneo mengi duniani, huku asimilia 57 ya watu wakiamini hali itakua mbaya zaidi ifikapo mwaka 2017.

Majengo ya baadhi ya maeneo ya nchi ya Yemen yaliyokumbwa na matukio ya ugaidi

Nchi nyingi za barani Ulaya, Marekani, Canada na Australia zimetajwa kuwa ni sehemu ambazo hazina hatari ingawa kuna baadhi ya miji ndani yake ina uwezekano mkubwa wa raia kupata matatizo.

Maeneo ambayo yametajwa kuwa na uwezekano mkubwa kutokea majanga ya ugaidi, magenge ya ujambazi na ubakaji, magonjwa ya milipuko na vita ni Mexico, Honduras, Colombia, Haiti, Papua New Guinea, Pakistan, Egypt, Nigeria na Algeria.

Wakati huo huo yametajwa maeneo ambayo ni salama zaidi duniani kuwa ni Norway, Sweden, Iceland, Switzerland, Slovenia na Denmark......                   ( kwa habar zaid tembelea blog hii.)

No comments:

Post a Comment