Monday, November 14, 2016

Mambo yakufahamu kuhusu mke wa Rais mteule wa Marekani Melania Trump

 


Melanie Trump ambaye ni mke halali Rais mteule wa Marekani Donald Trump, alizaliwa April 26,1970 mjini Novo Mesto Yugoslavia. Alizaliwa na kupewa jina la Melanija Knavs baadae akabadilisha kuwa Melania Knauss.
 melanie1
                                                                        Melania Trump


 Baba yake alikuwa anajishughulisha na biashara ya magari huku mama yake akiwa mwanamitindo na mtengenezaji wa nguo za watoto. Aliishi kwenye familia ya kawaida akiwa na mdogo wake wa kike mpaka  baadae alipogundua kuwa na kaka mkubwa ambaye baba yake alimpata kwenye mahusiano kabla ya kuwa na mama yake.
 melanie2

Tasnia ya urembo & Elimu
Alipofikisha maika 16 akaanza kujihusisha na mambo ya fashion na mitindo, baada ya miaka miwili akasajiliwa kwenye moja ya mashirika yanayojihusisha na mitindo huko Milan. Japokuwa alikuwa akiendelea na masomo katika chuo cha Ljubljana, aliacha shule ili aweze kuendeleza kipaji chake, ingawa Tangu mwaka 2006 Melanie amekuwa akisema alishamaliza Degree yake ya masomo ya Uhandisi chuoni hapo.

Mwanzoni alikuwa akifanya kazi mjini Milan na Paris kabla ya kuhamia New York mwaka 1996 ambapo ndipo alipopata makazi ya kudumu kikazi na aliweza kufanya kazi na wapiga picha maarufu kama Patrick Demarchelier na Helmut Newton huku akitokea kwenye kurasa za mbele za majarida makubwa ya fashion

 melanie6
                          Melania na Donald Trump kwenye harusi yao 2005 -Palm Beach Florida

Kukutana na Donald Trump mpaka  Ndoa
Mwaka 1998 Melania alikutana na Donald Trump huko New York katika party ya fashion, japokuwa mwanzoni alimtolea nje Trump, baadae wakaelewana na kuanza kuweka mahusiano yao hadharani na mwaka 2004 Trump akamvisha pete ya uchumba. Mwaka uliofuata 2005 wakafunga ndoa huko Palm beach Florida, sherehe ambayo ilihudhuriwa na mastaa wakubwa, pamoja na Rais Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton ambaye wakati huo alikuwa seneta kwenye jimbo la New York.

melanie-5

   Melania, Donald Trump na mtoto wao Barron


Mwaka 2006 Melania alijifungua mtoto wa kwanza, Barron William Trump ambaye kwa Trump yeye ni mtoto wa tano. Mwaka huo huo Melania akawa raia rasmi wa Marekani.

Wakati wa Kampeni za Urais
Wakati Donald Trump alipotangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi 2016, kama ilivyokuwa kwa Michelle Obama, Melanie alianza kujihusisha na jamii huku akipokea maoni mabaya yaliyokuwa yakihusisha picha za utupu alizowahi kupiga wakati akiwa model mwaka 2000 huku raia wakilalamika kuwa sio mfano wa kuigwa kwa jamii kutokana na picha zake nyingi za utupu zilizosambaa mitandaoni.

Maneno hayakuishia hapo, July 2016 Melania alitoa hotuba makao makuu ya chama cha Republican ambayo maelezo mengi yalifanana na yale ya Michelle Obama wakati alipokuwa akitoa hotuba yake 2008 makao makuu ya chama cha Democratic Marekani ambapo iliibua mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari.

melanie3 
July 2016 Melania Trump alipokuwa akitoa hotuba yake iliyofananishwa na ile ya Michelle Obama

Baadae mwandishi wa Trump Meredith McIver, akakiri kukosea na yeye ndiye alichanganya kwa bahati mbaya ripoti ya Melanie na baadhi ya maneno yaliyokuwepo kwenye hotuba ya Michelle. Mwezi huo huo july 30,2016 gazeti la Ney York Post likachapisha picha za utupu za Melania Trump akiwa na miaka 25, ambapo alionekana akiwa na mwanamke mwenzake, picha ambayo baadae ilifutwa.

Baada ya sekeseke hilo Trump aliwajibu The New York Post kuwa Melania ni moja kati ya models wenye mafanikio makubwa na amepiga picha nyingi kwenye covers za majarida makubwa na picha hiyo ilichapishwa kwenye jarida la Uingereza na ndilo lilimuwezesha kumfahamu Melania.

melanie-8 
Cover la jarida la Vogue baada ya harusi ya Melanie na Donald Trump

November 2016, Melanie alitoa hotuba fupi wakati wa kampeni na akieleza ni kitu gani atakachofanya ili kuzuia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kama atakuwa first lady wa Marekani na kusema kuwa ‘Tunapaswa tuwafundishe vijana wetu maadili ya kimarekani, wema, uaminifu, heshima, huruma, upendo, maelewano na ushirikiano’ 

Melania ana duka kubwa maarufu la vito vya thamani pamoja na bidhaa za ngozi.

melania-7 


Aidha ameshawahi kutangaza kipindi maarufu cha The View pamoja na kuonekana katika Reality Tv Show ya mumewe inayoitwa Celebrity Apprentice.

melanie7 
 Kingine kutoka kwa Mke wa Rais Mteule Melania Trump ni kwamba na uwezo wa kuongea vizuri lugha tano ikiwemo  Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kislovenia na Kiserbia.



No comments:

Post a Comment