Tuesday, November 15, 2016

Msanii Chemical: Mimi bado ni bikira

xchemical-jpg-pagespeed-ic-mwfnkzthan 
Rapper wa kike Bongo mwenye swagga za hatari, Chemical amefunguka na kusema yeye bado ni bikira (hajawahi kujigijigi tangu azaliwe).

Alisema hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha D’WIKEND CHATSHOW kinachorushwa kupitia Clouds TV
.
“Sijawahi kuwa na mahusino na mtu yeyote,” alisema.

“Siri ya kujitunza hadi leo hii kuwa bado nipo hivi ni kutokana na jinsi ambavyo nimelelewa maana mara nyingi nyumbani huwa tunaambiwa kuwa usifanye hivi na vile hadi uolewe, na mimi kwahiyo nimekuwa hivyo nikawa naogopa,” aliongeza.

Hata hivyo Chemical amesema licha ya kuwa bikira, hajawahi kujihusisha na mapenzi na wasichana wenzake (ulesbian).


No comments:

Post a Comment