Ahadi
nyingi zilitolewa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani ambapo sio
tu kutoka kwa Wagombea bali hata mastaa wakubwa waliokuwa upande Hillary
Clinton, wengi waliahidi kuondoka Marekani na kuhamia mataifa mengine
iwapo Donald Trump atashinda.
Tayari
matokeo yametangazwa November 9, 2016 na kuonyesha kuwa Donald
Trump ndiye mshindi na Rais mteule wa Marekani ambaye ataapishwa kuwa
Rais kamili wa taifa hilo January 20, 2017.
Mastaa watano walioandika watahama nchi ni hawa hapa kwenye hii orodha akiwemo mwimbaji Miley Cyrus yeye alisema “I am moving if he is president. I don’t say things I don’t mean!” ‘Nitaondoka kama Trump atakuwa Rais, huwa siongei vitu ambavyo simaanishi.’
Miley Cyrus
Mwimbaji staa wa RnB Ne-Yo alisema, “Like so many others, plans to bug out to nearby Canada” Kama wengine wengi, nina mpango wa kuhamia karibu na Canada“
Mwigizaji Samuel Jackson alisema “If that motherf***er becomes president, I’m moving my black a** to South Africa, Kama Trump atashinda uraisi nitahamia Afrika Kusini‘
Mwigizaji mchekeshaji Amy Schumer alisema “I will need to learn to speak Spanish, because I will move to Spain or somewhere.” Itabidi tu nijifunze kuongea kihispania kwa sababu nitahamia Hispania ama sehemu nyingine.
Mwigizaji Lena Dunham alisema “I know a lot of people have been threatening to do this, but I really will. I know a lovely place in Vancouver.” ‘najua watu wengi wametishia kufanya hivi lakini mimi nitafanya kweli, naifahamu sehemu moja nzuri huko Vancouver (CANADA)’
Rapper mkongwe Snoop Dogg
nae aliweka wazi utayari wake wa kuhamia CANADA na hata alipost picha
ya mnara wa Canada kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini alivyomtag
Drake ambae ni mzaliwa wa Canada.
Baada ya mastaa hao kuyaongea hayo, raia
wa Marekani wanasubiri kuwaona watafanya kweli baada ya Trump
kuchaguliwa kuwa raisi wa 45 wa Marekani.
No comments:
Post a Comment