Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake hapa nchini imetoa msaada wa shilingi bilioni 26.4 kusaidia wakimbizi walioko katika mikoa ya kanda ya ziwa kama vile Kigoma na Kagera.
Kwa mujibu wa Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Kochanke, fedha hiyo itatengwa mara mbili ambapo kiasi kitapelekwa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) na nyingine Shirika la Chakula Duniani (WHO).
“Fedha hizi tumezitenga kwenye mafungu haya kwa sababu kila shirika moja lina majukumu yake kwa wakimbizi, Mfano; WHO lenyewe ni kwa ajili ya kuhudumia chakula na UNHCR linashughulikia mambo mengine kama Afya na usalama,” alisema Kochanke.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba, alisema Tanzania kwa kushirikiana na nchi mbalimbali zinaendelea kushirikiana ili kuhakikihisha wakimbizi wanapungua.
No comments:
Post a Comment