Familia ya “Rais Mteule” wa Marekani Donald Trump inazidi kuzimiliki
headlines kubwa wakati ikijiaandaa kuingia Ikulu ya White House. Mbali
na nafasi aliyoipata mfanyabiashara huyo tajiri, Trump anaishi maisha ya
kifahari kwenye jumba lake lenye thamani ya shilingi za Tanzania zaidi
ya Bilioni 215.
Jumba hilo liko kwenye eneo lenye ukubwa
futi za mraba elfu themanini (80,000) ufukweni mwa jiji la Florida.
Trump alinunua jumba hilo kwa dola za Marekani Milioni 5 mwaka 1985 na
kulifanyia ukarabati ambapo sasa lina vyumba vya kulala 58, bafu 33,
jiko lenye meza za Marble kwa ukubwa wa futi 29, pamoja na sehemu za
kuwasha moto 12.
No comments:
Post a Comment