Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa Francis amesogeza mbele kwa muda usiojulikana suala la mapadre wa
kikatoliki duniani kusamehe wanawake walitoa mimba.
Hapo awali maaskofu peke yao ndio waliokuwa na uwezo wa kuwasamehe wanawake waliotoa mimba.
Baba mtakatifu amesisitiza kwamba mafundisho ya kikatoliki yanaonyesha kwamba utoaji mimba ni kosa kubwa, lakini kiongozi huyo ameeleza kwamba Mungu ni mwenye huruma na anaweza kusamehe dhambi zote ikiwa mkosaji atatubu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani amesema anaelewa jinsi suala la utoaji wa mimba linavyoweza kuwa tatizo kimaadili kwa mwanamke.
Toa maoni yako.
No comments:
Post a Comment