Tuesday, November 15, 2016
Duniani Nchi ambayo bado TV ya taifa haijatangaza chochote kuhusu ushindi wa Trump
Unaweza kufikiri mpaka sasa dunia nzima inafahamu kuwa Donald Trump ndiye raisi mteule wa Marekani lakini sio hivyo sababu kwenye taifa la Korea Kaskazini bado vyombo vya habari vya taifa mpaka sasa havijatoa habari yoyote ya ushindi wa Donald Trump kwenye Urais Marekani.
Mwandishi Chris Greenway wa BBC aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwa kusema ‘Leo ni Jumatatu hapa Korea Kaskazini ambapo mpaka sasa vyombo vya habari vya taifa havijawataarifu Wananchi wake juu ya matokeo ya uchaguzi nchini Marekani.’
Inasemekana kwa Korea Kaskazini sio rahisi kwa vyombo vya habari vya taifa kufanya hivyo kwani taarifa huwa zinachujwa na Wananchi hupokea habari zile tu ambazo serikali imezipitisha na sio vinginevyo.
Kwenye uchaguzi wa safari hii Marekani kwa Korea Kaskazini umekua tofauti na ule wa 2008 ambao Korea Kaskazini ilitangaza matokeo yake siku tatu baada ya Barack Obama kushinda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment